Rapa kutoka nchini Uganda Prezzo amesema hana haja na kolabo za wasanii
wakubwa wa Afrika kwani yeye ameshapewa baraka baada ya kukutana na Rapa
Jay Z.
Akizungumza na Enewz Prezo alisema kuwa yeye anajiamini hata
alivyokutana na Jay Z rapa huyo alionekana kufurahia uwepo wake hivyo
hana haja sana na kolabo za wasanii wa Afrika ili kutoka kimuziki.
Pia Prezzo alimpongeza msanii Jaguar kutoka nchini Kenya kwa kolabo yake
na Mafikizolo huku akimpa pole kwa kutojua kudab katika nyimbo hiyo
kiasi cha kukosea kufanya hivyo katika video yake.

Tagged with: ENTERTAINMENT
No comments :