NEWS

SPORTS

ENTERTAINMENT

VIDEOS

/ / Chid Benz akanusha kutoroka rehab, Adai kuwa ameruhusiwa

Msanii Chid Benz amekanusha taarifa zilizopo kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao kuwa ametoroka rehab Bagamoyo, alikokuwa akipata tiba ya kuacha madawa ya kulevya.

Video: Meneja wa 'Sober House' akielezea juu ya Chidi Benz kutoroka kaaba ya siku 28 tu!

Akiongea na East Africa Radio Chid Benz amesema si kweli kwamba ametoroka, isipokuwa ameruhusiwa kutoka rehab.

"Wameongea uongo hao wajinga, nimeachana nao kwa sababu hatuwezi kubishana nao, mi nimetoka niko sawa, nipo fresh na siwezi kubishana na magazeti, na sasa hivi nipo studio nataka niingie kurekodi, kwa hiyo sio kweli kama nimetoroka rehab, nimetoka kwa sababu nimeruhusiwa", alisema Chid Benz.

Hata hivyo East Africa Radio iliamua kumtafuta mtu wa karibu wa Chid Benz (Madee) ambaye naye yupo chini ya Babu Tale, na kuthibitisha taarifa hizo kuwa hajatoroka kweli.

Chid Benz alipelekwa rehab Bagamoyo mwezi wa 3 mwaka huu, baada ya meneja wa TipTop kujitolea kumsaidia kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, ambayo yalikuwa yameshamuathiri.

«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post

About B45

Asante kwa kutembelea BENSON 45,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA BENSON45.BLOGSPOT.COM.

No comments :

Leave a Reply