NEWS

SPORTS

ENTERTAINMENT

VIDEOS

/ / Gabo:Mimi ni zaidi ya Ray

Msanii wa filamu nchini ambaye anafahamika kwa kuigiza kwa lafudhi ya Kimakonde Gambo Zigamba amefunguka na kusema kuwa yeye ni zaidi ya msanii Ray Kigosi kwenye kazi kwani yeye anafanya zaidi ya Ray.

Akizungumza kwenye kipindi cha eNewz Gambo Zigamba aliweka wazi kuwa kipindi ambacho wakina Ray na wasanii wengine wakongwe wanafanya kazi zao hizo kulikuwa hakuna wasanii wengine wachanga ndiyo maana walikuwa wanaonekani ni wazuri sana lakini hivi sasa tasnia imekuwa na vipaji vipya ambavyo vinafanya vizuri zaidi yao hao wakongwe.

Mbali na hilo msanii huyo alikubali kuwa msanii Ray Kigosi ana ladha zake katika kazi na ana mashabiki wake katika tasnia hiyo ila anachoamini yeye ni zaidi ya Ray Kigosi na kusema wapo watu wana uwezo wa kufanya kitu zaidi ya huyo Ray.

"Ray ana flavor (ladha) zake na wapo watu wapo wanampenda Ray lakini kuna watu zaidi ya Ray wanaweza kufanya vizuri zaidi ya Ray, ila naweza kusema mimi ni zaidi ya Ray kwani naweza kufanya kitu zaidi ya Ray, Ray akabaki amefanya na mimi nikafanya zaidi yake na watu wakapenda zaidi. Mimi siogopi mtu japo ukweli utabaki pale pale kuwa baba ni baba ila mtoto anaweza kufanya jambo vizuri hata zaidi ya baba yake," alijigamba Zigamba.

- EATV

«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post

About B45

Asante kwa kutembelea BENSON 45,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA BENSON45.BLOGSPOT.COM.

No comments :

Leave a Reply