Mwanamitindo na Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amefunguka juu ya ugomvi wa Mirror na Petiti Man.
Akizungumza na Enewz Kadinda alisema
kuwa ugomvi wa Mirror na Meneja wake anayesimamia kazi zake za muziki
yaani Petit man ni utoto tu unawasumbua.
“Petiti
bado yupo Endles Fame kwakuwa bado hajaiandikia barua kampuni kuwa
anatoka na yote yaliyotokea kati ya petit na Mirror ama Wema ni tofauti
zao tu kawaida ambazo si mara ya kwanza kutokea”,alisema Kadinda.
Hapo awali Mirror aliiambia Enewz kua
hasimamiwi tena na Petit katika kazi zake huku Petit akitaka tumuulize
Meneja wa kampuni ambaye ni Kadinda juu ya swala hilo kwakuwa yeye ndo
msemaji wa kampuni hiyo.
No comments :