Kuna taarifa sinazosambaa kua malkia wa
label ya Mavin Records chini ya mwanamuziki Don Jazy, Tiwa Savage
anategemea kuingia mkataba mpya na label ya mwanamuziki Jay Z
inayojulikana kama “Roc Nation”.
Kwa sasa Tiwa Savage anapewa uangalizo
wa karibu sana na Jay Z na yupo tayari kuingia mkataba na malkia huyo wa
Mavin Records chini ya label yake hiyo ya Roc Nation.
Kwa mujibu wa vyambo mbali mbali vya
habari Nigeria vinasema kuwa Jayz ameonekana kushangazwa na wasifu wa
mwanandada huyo na aliamuru kuanzisha taratibu hizo za kumuingiza Tiwa
Savage katika label yake akiwa na Briant Biggs na Shawn Pecas.
Roc Nation ni label kubwa huko Marekani
ikiwa inafanya kazi na wasanii wakubwa kama Rihanna, Big Sean, Dj
Khaled, J.cole na wengine wengi tu.
Tiwa tayari ameshapangiwa kufungua
katika tamasha la Rihanna litakalo fanyikwa mwezi wa tisa mwaka huu huko
Marekani. Na kwasasa hiki ndicho anachokihitaji mwanadada huyo hususani
baada ya kua kwenye matatizo na ndoa yake.
Bado tunasubiri uthibitisho juu ya hiki kinachosemekana kinaendelea kutoka kwa muhusika mwenyewe Tiwa Savage.
No comments :