Kanye West na Jengo La Dola Million 11 Kwa maandalizi Ya Familia Mpya
Pichani Ni Rapper kanye West A.K.A Yeezy Akiwa na Mpenzi Wake Kim kardashan Katika pozi
Pichani Ni Jumba Walilonunua Kanye na Kim kardashan
Ambalo limewagharimu kiasi cha Dola Za kimarekani Million 11 , Jumba
Hilo Lililopo katika eneo la gated Bel Air, California, Kwa hela za
Tanzania ni sawa na Shilingi za Kitanzania Billion 16 , Jumba Hilo
Linakadiriwa kuwa na ukubwa wa Mita Za Mraba 10,000 pamoja na bwawa
Kubwa La kuogelea, Sehemu Ya Kufanyia Mazoezi Yaani Gym , Kiwanja Kidogo
cha Mpira wa kikapu na pia Bwawa la kuogelea la ndani ya Nyumba Maarufu
kama Indoor Pool ,inasemekana jumba Hilo limedizainiwa kwa muundo wa
majumba za kiitaliano, Kwa Ajili Ya Familia Yao Wanayotarajia kuipata
baada ya Miezi Tisa. Hawa ni baadhi ya Mastaa Wenzao ambao ni Majirani
Wao wa Karibu Jennifer Aniston na Mcheza Kikapu Chris Paul.
Wapenzi Hawa Ambao Tangu Waingie kwenye Uhusiano wao
wamekuwa wakiandikwa kwenye Vyombo Mbalimbali Vya Habari Kuhusiana na
Mahusiano yao , ambao Bi Mdada kim Kardashan Alivunja Ndoa yake Na
Mcheza kikapu Chris Humphreys Iliyodumu kwa muda wa siku 72 Na kuhamisha
Makazi Kwa Rapper kanye West, Na hivi juzi juzi Vyombo Vya habari
Vilimnukuu Kim K pamoja na kanye west kwamba Bi Mdada huyo tayari
ameshika Ujauzito Na ivyo Wanajiandaa Kumpokea mtoto kama ilivyo kwa
mastaa wengine kama jay z na beyonce.
No comments :