“Nasikiaga uzuri wa
nyumba usikufanye utembee peku, sista duu usitoe mimba kesho ulie kama
Wema Sepetu,” anaonekana Harmonize akirap na kushangiliwa na washkaji
zake. Video hiyo imesababisha hasira kubwa kwa mashabiki wa Wema
waliomporomoshea matusi usiku kucha kuanzia jana.
Wema aliupata ujumbe huo na aliamua
kuujibu kwa busara zaidi kwa kuweka nukuu ya Angelina Jolie kwenye picha
hiyo chini na kuandika tu: Well. Arent you??”
Wema alijibu pia lakini kama kawaida kwa utani mwingi.
“As i sit here nikakumbuka kitu “Jamani
nimeanzisha format yenye ustaarabu na taratibu, kwa yoyote anayetamani
kutafuta kiki kupitia mimi kuna contract nimeandaa ni makubaliano mimi
na wewe kwa percent ya mapato utakayopata kwa kiki hiyo ili itunufaishe
wote tena ntakupa hadi na idea za jinsi ya kunitukana na kunimaliza
kwasababu najua mwisho wa siku tunavuta mpunga wetu wanashangaa kesho mi
na wewe tunacheka tu” hii naiita #MoneyKick #KikiPesa clients wote
email me bei ni maelewano,” aliandika.
Katika kujaribu kuliua soo, Harmonize
alijirekodi voice note na kuituma kwa makundi ya WhatsApp ya WCB lakini
snitch mmoja aliivujisha na kuiweka Instagram. Kwenye sauti hiyo
Harmonize anasikika anasema kuwa siku wanarekodi video hiyo aliomba
isisambae kwakuwa aliamini ingekuja kumletea matatizo.
“Bahati mbaya imetokea hatujui nani
amevujisha video imeleak,” anasema. Anadai kuwa mkakati waliojadili
kufanya ni kuipigia promo ngoma mpya ya Raymond ‘Natafuta Kiki’ ili
kumaliza nguvu ya video hiyo.
Kitu anachotakiwa kukifahamu Harmonize
sasa ni kuwa kile kinachojadiliwa kwenye magroup ya WhatsApp ya WCB
hakibaki humo tu, kuna snitches kibao wanaoweza kuumwaga mchele kwa
ndege wengi hasa wasiohusika!
No comments :