
March 8
2016, Serikali kupitia bodi ya sukari Tanzania, ilitangaza viwango vipya
vya bei ya sukari nchini vinavyoanza kutumika kuanzia sasa, akiongea na
waandishi wa habari Mkurugenzi wa bodi ya sukari Tanzania Henry Semwanza amesema>>
Serikali,
kupitia bodi ya Sukari Tanzania, inawaarifu wananchi wote kuwa bei ya
rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja‘
‘wafanyabiashara
wote wanapaswa kuzingatia agizo hili, pamoja na kuhakikisha kuwa sukari
inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi bila kuihodhi‘
‘Maafisa
biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na kusimamia utekelezaji wa
agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na hawatasita kuchukua hatua stahiki
za kisheria kwa wale watakaobainika kupandisha bei ya bidhaa hiyo‘
No comments :