NEWS

SPORTS

ENTERTAINMENT

VIDEOS

/ / Kundi la Islamic state lateka vijiji Syria

Image copyrightAP
Image captionIslamic state
Kundi la Islamic State nchini Syria limeteka vijiji kadhaa kutoka katika makundi hasimu ya wapiganaji kaskazini mwa mji wa Aleppo licha ya mashambulizi ya angani kutoka kwa jeshi la Urusi, ambapo Moscow inasema ilikuwa ikilenga kundi hilo.
Mwandishi wa BBC katika eneo hilo amesema kuwa licha ya madai ya Urusi kwamba inawalenga wapiganaji wa IS,Inaonekana kwamba kuyalenga makundi mengine ya waasi ambayo ni tishio kwa serikali ya Syria ambayo inaungwa mkono na Mascow.
Anasema kuwa kampeni ya mabomu inayotekelezwa na Urusi imeyadhoofisha makundi hayo na hivyobasi kutoa fursa kwa IS kusonga mbele.Wakati huohuo Kamanda mmoja mkuu wa walinzi wa kikosi cha mapinduzi nchini Iran, ameuwawa, baada ya kwenda kuwapa ushauri wanajeshi katika harakati zao za kukabiliana na kundi la Islamic State nchini Syria.
Iran inasema kuwa Jenerali Hussein Hamedani aliuwawa siku ya Alhamisi wakati wa ujumbe wa ushauri kaskazini mwa mji wa Aleppo.
Image copyright
Image captionJenerali Hamedani
Jenerali Hamedani alijadiliwa katika vikwazo vya jumuia ya bara Ulaya dhidi ya baadhi ya viongozi wa Iran baada ya kuhusika katika kuukandamiza upinzani baada ya matokeo tata ya uchaguzi wa Urais uliofanyika mnamo mwaka 2009.
Ni miongoni mwa makamanda wa jeshi wa Iran ambao wameuwawa huko.
Iran imekuwa ikiisaidia pakubwa utawala wa Rais Asaad wa Syria, tangu mapigano ya wenyewe kwa wenewe yalipoanza.

«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post

About B45

Asante kwa kutembelea BENSON 45,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA BENSON45.BLOGSPOT.COM.

No comments :

Leave a Reply