• Msikilizaji mzuri wa muziki wa hiphop utakuwa na ufahamu kuhusu wimbo #STAN wa Eminem&nb...

  • Rich Homie Quan atahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kama atakutwa na hatia kwenye ...

  • BET wametoa orodha ya wasanii ambao watapanda katika steji ya utoaji tuzo usiku wa June 2...

  • Chance the Rapper’s impact on Chicago continues to shine. Following the hometown hero’s $...

NEWS

SPORTS

ENTERTAINMENT

VIDEOS

/ / Rostam Aziz Atoa Ya Moyoni Kuhusu Kauli Ya Dr. Slaa

Mfanyabiashara maarufu Rostam Aziz amejitokeza na kujibu madai yaliyotolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dk Wilbroad Slaa kupitia mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika jana jijini Dar es salaam.Akizungumza na Waandishi wa Habari Dkt. Wibroad Slaa alidai kupata vitisho dhidi ya maisha yake kutoka kwa Bwana Rostam wakati alipotoa orodha ya watuhumiwa wa ufisadi Mwembeyanga jijini Dar es salaam



.
Kwa mujibu taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari na Rostam Azizi amedai kuwa tuhuma hizo zinadhihirisha wazi hulka aliyodai kuwa ni ya upotoshaji ambao umekuwa ukifanywa mara nyingi na Dk Slaa, na kuongeza kuwa kama kweli angalikuwa ametoa visitisho hivyo inashangaza kwa nini mlalamikaji hakufikisha taarifa hizo polisi.
Aidha, Rostam amemtaka Dkt Slaa kujitokeza hadharani na kutoa ushahidi wake dhidi yake kuhusiana na tuhuma hizo na kutaka wananchi wapuuze kile alichokiita uzushi.
Hata hivyo Rostam amekanusha kauli ya Dkt Slaa kwamba anaisadia Chadema ambapo pia amemtaka Dk Slaa kutoa ushahidi kuhusiana na suala hilo huku akikumbusha kwamba mwaka 2010 Dk. Slaa alimtuhumu kwamba akiwa yeye, Rais Jakaya Kikwete na Edward Lowassa walikutana katika hoteli ya la Kairo Mwanza kupanga njama za kumuibia kura zake za urais madai ambayo amedai hayakuwa na ukweli.
Amemtaka Dkt. Slaa kama mtu aliyekula kiapo cha upadri kuwa mtumishi wa Mungu kuepuka taarifa alizodai kuwa za upotoshaji zisizo na ukweli.
-sondacomblog

«
Next
Msanii Jux Afuguka Ya Moyoni Jinsi Vanessa alivyoyabadili maisha yake toka waingie kwenye Uhusiano.
»
Previous
NGASA ASEMA HAUELEWI MUSTAKABALI WAKE FREE STATE

About B45

Asante kwa kutembelea BENSON 45,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA BENSON45.BLOGSPOT.COM.

No comments :

Leave a Reply