Nidhamu ni kitu kikubw sana kwenye kila sekta duniani kote.
Cha kujiuliza ni Je Unaitambua thamani ya nidhamu katika kipaji chako ulicho nacho?
Vijana wengi wenye vipaji hasa chipukizi wamekuwa wakifeli kufikia malengo yao kwasababu tu ya kukosa nidhamu,Nidhamu haina mkubwa wala mdogo bali nidhamu ni moja ya njia yako ya kukupeleka katika mafanikio.
Nakumbuka siku moja nilikutana na kijana mmoja mwenye kipaji cha kuimba,akaniambia kuwa amekuwa akikosa nafasi za kuonyesha kipaji chake kila anapoenda,Kabla ya kumjibu chochote nilijiuliza hivi nini inaweza kuwa sababu ya kijana huyu kukosa nafasi?
Nilichomjibu nilimuuliza ni jitihada gani umefanya ili kupata nafasi ya kuonyesha kipaji chako?Akanijibu nimerekodi kwenye studio nzuri na nimefanya kazi na prodyuza mkubwa ambaye nimemlipa hela kubwa sana.
Swali lingine nikalipata kichwani kwani kufanya kazi na studio kubwa na prodyuza mwenye jina kubwa vinatosha kukufanya kuwa msanii mkubwa?
Mwisho nikatambua kuwa labda hawa wasanii wetu bado hawajajua vingi kuhusu thamani na kuthamini.
![]() |
Mtangazaji wa Metro Fm Mwanza,B forty five. |
Alivyoondoka yule kijana,kuna rafiki mmoja alikuwa pembeni akaniambia huyo dogo anadharau na hana nidhamu kila anapoenda,kuanzia katika vyombo vya habari mpaka kwenye maisha ya kawaida.
Hapo sasa ndo nilipogundua kuwa nidhamu inaweza kukufanya uthaminike au usithaminike kwa maana hiyo kama yule kijana angekuwa na nidhamu basi angepata nafasi ya kipaji chake kuonekana na hata wanaomzunguka wangemthamini sana tu.
Nimtolee mfano mtu kama Diamond Platnumz ni msanii mkubwa sana Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania,Lakini unapokutana nae unaona jinsi alivyo na nidhamu na kila unamuona kama ni msanii mchanga hii inazidi kumpa heshima na kumfanya aonekane anajitambua na kujielewa.
Leo hii Lil Wayne anaeonekana amedata kwa matumizi ya marijuana lakini inapofikia swala la nidhamu anaonyesha yupo sawa,mfano mzuri ni kwenye ile kauli yake kuhusu Black Lives Matter alipogundua amekosea ameamua kuomba radhi.
Kwa hili dogo la leo unaweza kujifunza kitu na kubadilisha mfumo mzima wa maisha yako ya sanaa,Kipaji bila nidhamu ni kovu.
No comments :