NEWS

SPORTS

ENTERTAINMENT

VIDEOS

/ / UKAWA YAPOTEZA MASTAA WAWILI KUTOKA BONGO MOVIE WAAMUA KURUDI CCM


Katika tasnia ya Bongo Movie Aunt Ezekiel na Vicent Kigosi 'Ray' (pichani hapo juu) wao hapo awali walikuwa wakionesha mapenzi yao kwa UKAWA, lakini hivi sasa wamegeuka na kuhamia CCM.
Wakizungumza juu ya kuhama huko kupitia 'Take One' ya Clouds Tv inayofanywa na Zamaradi Mketema 'Ray' alisema si ajabu yeye kuhama kutoka UKAWA na kurudi CCM kwani kwa sasa hilo si jambo la ajabu kwani kama mawaziri wakuu waliweza kuvihama vyama vyao haoni ajabu yeye kuhama kutoka UKAWA na kurudi CCM..
Aunt Ezekiel alipokuwa UKAWA kabla ya kuhamia CCM

"Lazima ufanye kazi ili upate mabadiliko kwa hiyo nimeona ni vema niungana na hawa wanaofanya kazi ii kutetea mabadiliko kuliko kuhitaji mabadiliko bila kufanya kazi naamini huku ambapo nimerudi nitapata mabadiliko yakutosha kupitia kazi nitakazofanya" alisema Aunt Ezekiel.
Stori za siasa kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka huu ni nyingi sana kiukweli na tumeshuhudia watu ,aarufu nchini wakionesha mapenzi yao kwa vyama na wagombea wanaowaamini.
Kwa upande wa Aunt Ezekiel yeye kupitia kipindi hicho alisema kazi kwanza mabadiliko baadaye kwani anaamini ukifanya kazi mabadiliko yatafuata hapo baadaye kutokana na juhudi za kufanya kazi, huku akimuomba mgombea urais kupitia Chama cha Mapindizu CCM , Dk John Magufuli kuikumbuka tasnia hiyo pindi atakapofanikiwa kuwa rais.

«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post

About B45

Asante kwa kutembelea BENSON 45,NITAKUHABARISHA, KUKUELIMISHA NA KUKUBURUDISHA HIVYO USIKOSE KUTEMBELEA BENSON45.BLOGSPOT.COM.

No comments :

Leave a Reply