MWANAMUZIKI kutoka Marekani Chris Brown, ambaye hivi sasa ametupwa
rumande anadaiwa kuwa ataruhusiwa kuoga mara moja tu ndani ya siku mbili
akiwa jela.
Mwanamuziki huyo wa miondoko ya R&B, alitupwa jela wiki hii ambako atakaa kwa mwezi mzima baada ya kufukuzwa rehab.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umedai kuwa Brown atafungiwa kwenye chumba
chake pekee yake kwa zaidi ya masaa 23 kila siku, ingawa ataruhusiwa
kusoma vitabu pamoja na kufanya mazoezi.
Ambapo atakaa jera hadi 23 April, ambapo ametolewa Rehab baada ya
kufanya vitendo vinavyoenda kinyume na sheria ya rehab ikiwa moja wapo
kumshika mwanamke kinyume na masharti ya huko.
Brown ameponzwa na tabia yake ambapo, alimshika mwanamke kinyume na
masharti ya humo pamoja na kukaataa kuchukua vipimo vya dawa ya kulevya
na kwa kutoa kauli za vitisho wakati wa 'therapy' ya kundi kwa kudaiwa
kusema kuwa 'i am good at using guns and knives'.
No comments :